Jifunze computer programming kwa kiswahili:1
Jifunze kuhusu COMPUTER PROGRAMMING kwa lugha ya Kiswahili: 1
Je! Umewahi kusikia kuhusu computer programming? Na umewahi
kujiuliza ni vipi vifaa hivi vya kielectronic vinavyofanya kazi?
Watu wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kujua kuhusu
computer programming ila kutokana na vikwazo mbalimbali malengo yao huishia
njiani, miongomi mwa vikwazo wanavyokutana navyo ni pamoja na vifaa vya
kujifunzia, pesa, lugha( language barrier) n.k
Katika kurasa hii nitajaribu nkuzungumzia kuhusu computer programming
ila kabla ya kuendelea kuna maneno ambayo unatakiwa kuyajua ili
yasikuchanganye.
PROGRAM ni mkusanyiko wa
maelezo (instructions) ambayo yanaipa au kuiamrisha computer kazi ya kufanya,
computer inahitaji program ili uweze kuitumia, bila ya program(s) computer
haiwezi kufanya kazi unazoziona ikifanya na computer bila ya program(s) ni sawa
na ndege isiyokuwa na rubani.
Nitatoa mfano ili
upate kunielewa vizuri, ni mara nyingi sana umewahi kukutana na maneno kama
vile calculate, paste, login, delete n.k maneno hayo ndiyo maelezo ( instructions) niliyoyakusudia,
ambapo maelezo hayo yanakuwa yameandikwa kwa programming languages ambapo
baadaye yanabadilishwa na kuwa katika mfumo wa binary(machine language) ili
computer iweze kuyaelewa (nitaelezea iko vipi).
marks=int(input("Enter your marks: "))
if marks<50:
print("YOU
FAILLED")
else:
print("YOU PASSED")
Huu ni mfano wa maelezo (instructions) ulio andikwa kwa
lugha ya python programming language ambao una mtaka mtumiaji (user) kuingiza
marks zake, ila hapo kuna neno print
ambalo hili ni mfano wa maelezo (instruction) ambalo linaiambia computer
kuonyesha matokeo (print) na maelezo hayo ndiyo tunayaita code.
SOFTWARE najua kuna watu
wanajiuliza je! Kuna tofauti gani baina ya program na software? Jibu ni kuwa
program ni mkusanyiko wa maelezo ambayo yaniambia computer ifanye nini mfano:
delete, copy, save ,print n.k lakini software ni mkusanyiko wa programs ambazo
zinatengeneza kitu kimoja(software) ambayo inafanya kazi maalumu.
Aina za software
Kuna aina mbili za software ambazo ni
v
System
sofrware mfano
wake ni operating system, utility
programs na device driver
v
Application
software mfano wake ni word
processing(MS Word/Word perfect), vlc,
Adobe, Chrome n.k
COMPUTER PROGRMMING hiki
ni kitendo cha kubuni na kuandika
maelezo(instructions or codes) ambayo yatatengeneza program kwa ajili ya
kukamilisha kazi maalumu.
PROGRAMMER(CODER,DEVELOPER OR SOFTWARE ENGINEER) huyu si mwingine bali ni mtu kama mimi na wewe
ambaye anafanya kazi ya kutengeneza
computer software kwa kutumia codes(instructions).
PROGRAMMING LANGUAGES hizi ni lugha ambazo hutumiwa na programmer
wakati wa kutengeneza program. Programming languages ni lugha ambazo
zimekusanya misamiati(maneno) ambayo ndani yake ndio kuna maelezo(
instructions) yanayo iambia computer au kifaa kingine cha kielectronic kufanya
kazi maalumu. Mfano wa maneno hayo ni kama, print,if,not, and,range do, case
then n.k
Aina za computer programming languages
v
Low level
language : hii ni
lugha ambayo hutumiwa na processor ili
kuweza kufanya mawasiliano na hardware katika mfumo wa computer, programmer
hutengeneza program kwa kutumia high level language ambapo ili computer iweze
kuelewa imeambiwa nini ni lazima lugha hii iweze kubadilishwa kutoka katika
high level language na kuwa katika mfumo wa low level language (binary format)
Mfano: programmer akiandika neno ADD ambalo neno hili lipo katika high level
language na neno hili likisafirishwa kupelekwa katika microprocessor kwa ajili
ya matumizi, computer haiwezi fahamu kuwa imeambiwa ifanye nini, hivyo basi ni
lazima neno hili liweze kutafsiriwa au kubadilishwa na kuwa katika mfumo wa low level language,
low level language ni mfumo wa binary ambao huwa ni 0 na 1, mfano neno ADD
linabadilishwa na kuwa katika low level language litasomeka kama 110011(mfano), kumbuka kuwa computer inaelewa
0 na 1 tu na sio A,B,C,D …..Mfano wa low level language ni Machine language na assembly language.
v
High
level languages : hizi ni lugha zinayotumiwa na programmers ambazo zina wazesha kuandia program ambayo
mara nyingi haitegemei aina ya computer, programmer ni vyepesi kwao wao kuweza kuzifahamu lughahizi ila ni ngumu kwao
kuifahamu low level language, vivyo hivyo ni vigumu computer kuweza kuzifahamu lugha hizi
za high level tofauti na low level language. High level languages haziwezi kuingiliana
na mfumo wa hardware katika computer, high level programs zinahitaji compiler/interpreters ili ziweze kutafsiri source code kutoka katika
high level landuage na kuwa low level language
Zingatia: low level language ni
lugha ya computer na high level language ni lugha anayotumia programmer
kutengeneza program
Mfano wa high level languages ni kama vile Java, Phython, Pascal ,C++, Cobol, Ruby,
Javascript, Php, Html n.k
|
Faida za low level language(machine
language)
v
Ufanyaji kazi (running) wa low level language ni
wa haraka zaidi kuliko high level language kwa sababu lugha hii haihitaji
kutafsiriwa tena, hivyo ikifika kataka microprocessor hufanyiwa kazi moja kwa
moja bila kutafsiriwa tena, tofauti na high level language ambapo ni lazima
itafsiriwe kwanza ili iwe katika low level language ili iwezwe kufanyiwa kazi na
microprocessor.
v
Inaweza kuwasiliana moja kwa moja na hardware
Hasara za low level languages(machine languege)
v
Programs zilizotengenezwa kwa low level language mara nyingi hutegemea na aina ya computer na vile vile haziwezi kuhamishkia kutoka kifaa kimoja (computer)kwenda kingne, kwasababu zinakuwa zinategemea microprocessor
v
Programs
zilizotengnezwa kwa low level language ni ngumu sana kuziendesha na
kuzirekebisha hata kutafuta tatizo(error) ni ngumu sana, kwa sababu programmer
anakuwa na ugumu wa kuifahamu lugha hii.
v
Programs zilizotengenezwa kwa low level language
mara nyingi huwa ni error prone.
Error prone maana yake
ni kuwa program hiyo ni nyepesi sana kufanya error
Faida za high level language
v
High level language ni rafiki sana na
programmer, kwani programmer ni vyepesi sana kuielewa high level langiuagr
tofauti na low level language.
v
Ni vyepesi sana kwa programmer kuiandika (write),
kuondoa error (debug) na kufanya marekebisho mengine.
Debugging (debug) ni mchakato au hatua (process) za kutafuta na kuondoa
error katika program.
Debugger hii ni software inayotumika kuangalia kama kuna error katika program na kuweza kuiondosha.
v
High level language hazitegemei aina ya
computer, hivyo basi hata ukiihamisha inaweza kufanya kazi katika kifaaa kingine
tofauti na low level language.
v
High level language sio sana kufanya error(less
error prone)
Hasara za high level language
v
Ina hitaji muda mwingine ili kuweza kutasfriwa
kutoka katika high level language na kuwa low level language
v High level language haiwezi kuwasiliana na
microprocessor moja kwa mooja mpaka itafsiriwe kuwa low level language
v
High level language ufanyaji kazi wake si wa
haraka sana kama low level language.
........ to be continue
Katika darasa linalofata nitajaribu kuzungumzia baadhi ya vitu nilivyo viacha, mpaka kufikia hapo mimi sina la zaidi, kama una maswali au maoni dondosha hapo katika comment........
By Djmuba_+255769631203
Unguja_ Zanzibar
nimependa somo lako, kuna kitu nasubir huenda kwenye somo lijalo kitakuwepok . vinginevyo nitauliza.. . .
ReplyDelete